Nani kuvaana na Madrid fainali ligi ya mabingwa?


Shangwe zimetawala mitaa ya  Madrid baada ya timu hiyo kufuzu  fainali ya Ligi ya mabingwa kwa mara ya 16 mtawalia na mkufunzi wa timu hiyo  Zinedine Zidane akiwa kocha wa kwanza kuipeleka Madrid katika  fainali hizo mara 3 hizo baada ya Marcelo Lippi  mwaka 1996-1998.

Pamoja na  kutoka sare ya mabao 2-2 na Bayern Munich usiku wa jana katika mchezo wao wa marudiano, Real Madrid imefanikiwa kusonga mbele kwa hatua hiyo kutokana na faida ya ushindi wa magoli 2-1 iliopata kwenye mechi yake ya kwanza ya hatua ya nusu fainali na wapinzani wake hao.

kwa ushindi huo, Real Madrid  wanasubiri kujua ni nani atakayekutana nae fainali ambapo usiku wa leo nusu fainali ya pili itashudiwa pakubwa kule italia.

AS Roma atamualika  Liverpool na mchezo katika mchezo wao wa awali Liverpool waliibuka na ushindi wa Mabao 5-2 dhidi ya AC Roma.

Post a Comment

Previous Post Next Post