Wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika, Yanga SC wanatarajiwa kuondoka nchini leo Mei 03 kwa ajili ya mchezo wao wa kwanza wa kombe hilo Barani Afrika dhidi ya USM Alger nchini Algeria.
Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa timu hiyo Dismas Ten amesema kwa sasa nguvu zote wanaelekeza katika mchezo wao wa kombe la Shirikisho ili kuhakikisha wanafanya vizuri kwenye mechi yao ya kwanza dhidi ya USM Alger.
Yanga wataondoka nchini kupitia Dubai na baadae kuelekea nchini Algeria ili wawahi kufika nchini humo sambamba na kuzoea hali ya hewa.
kwa sasa Yanga inayosimamiwa na kocha msaidizi Shadrack Nswajigwa imekua ikipata matokeo ya kususua tangu alipoondoka aliyekuwa kocha mkuu wa timu George Lwandamina.
Yanga ipo kundi ‘KUNDI D’ pamoja na U.S.M Alger, Rayon Sports na Gor Mahia FC na wamefuzu katika hatua ya makundi baada ya kuiondosha Welayta Dicha SC ya Ethiopia kwa jumla ya mabao 2-1.
