Alijipatia kipato cha $275m (£205m) katika mechi
yake ua masumbwi mwezi Agosti dhidi ya nyota wa UFC star Conor McGregor, ambaye
yuko nambari nne katika orodha ya jarida hilo la biashara nchini Marekani.
Cristiano Ronaldo ambaye alikuwa akiorodheshwa wa kwanza
katika kipindi cha miaka 2 iliopita sasa ni wa tatu huku Lionel Messi akichukua
wadhfa wa pili kwa tofauti ndogo.
La kushangaza ni kwamba hakuna wanawake katika
orodha hiyo baada ya mwanamke wa pekee katika orodha hiyo Serena Williams
kutoorodheshwa.
Wanamichezo 10 tajiri zaidi duniani.
1. Floyd Mayweather - Ndondi
($285m)
2. Lionel Messi - Kandanda ($111m)
3. Cristiano Ronaldo
-kandanda($108m)
4. Conor McGregor - Karate, judo na
Ndondi ($99m)
5. Neymar - kandanda ($90m)
6. LeBron James - Vikapu ($85,5m)
7. Roger Federer - tenisi ($77.2m)
8. Stephen Curry - Vikapu ($76.9m)
9. Matt Ryan - Soka ya Marekani
($67.3m)
10. Matthew Stafford - Soka ya
Marekani ($59.5m)
Chanzo: BBC Swahili
