Ferooz ataja siri ya kutorudi kwenye muziki


Na. Aminah Kasheibar

Mkongwe wa muziki wa bongo fleva, Ferooz Mrisho ametoa Siri ya yeye kutokurudi kwenye soko la muziki.

Ferooz ambaye alitamba na wimbo 'Starehe' ambao ulifanya vizuri kwenye stesheni mbalimbali, amesema sababu ya yeye kuacha muziki au kutorudi kwenye game ni kutokana na watu kumcheka na kumdhihaki.

Alisema alijaribu kurudi lakini watu walimuona kama kituko vile wakati yeye alikuwa amerudi rasmi katika muziki.

"Inauma pâle unajaribu kufanya jambo fulani harafu watu wanakuona kama kituko mimi ni msanii wa kitambo natakiwa kupewa heshima kubwa kurudi kwangu ilikuwa ni kuja kufanya vizuri kama hapo awali.

"Sioni sababu ya kurudi tena ikiwa naonekana mtu nisieleweka hakuna kitu kinauma kama kuona kituko," alisema Ferooz.

Hata hivyo Ferooz amesema muziki wa sasa unaushindani mkubwa sana ambao unatakiwa kuwa mbunifu ili iweze kuteka mashabiki.

Post a Comment

Previous Post Next Post