Mbunge wa Nzega, Hussein Bashe amepata pigo baada ya kuondokew
na mama yake mzazi, Zainab Abdi.
Mama Bashe amefariki dunia leo katika Taasisi ya Moyo ya
Jakaya Kikwete iliyoko Hospitali ya Taifa Muhimbili, jijini Dar es Salaam.
Taarifa hizo amezithibitisha Bashe kupitia akaunti yake ya
mtandao wa kijamii wa Twitter.
“Ndugu zangu nimeondokewa na mama yangu mpendwa, Inna
Lillahi wa inna ilayhi raji’un," ameandika Bashe katika ukurasa wake wa Twitter.
