MKUTANO Mkuu wa mwaka wa klabu ya Yanga SC uliokuwa umepangwa kufanyika Jumamosi Juni 17, mwaka huu umerudishwa nyuma kwa wiki moja hadi Juni 10 na utafanyika mjini Dar es Salaam katika ukumbi ambao utatajwa baadaye.
Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa ameiambia Bin
Zubeiry Sports – Online kwamba hayo yamefikiwa katika kikao cha Kamati ya
Utendaji kilichofanyika jana mjini Dar es Salaam na katika mkutano huo
wanachama wa kadi zote wataruhusiwa kuingia – tu wawe wamezilipia.
“Kadi za uanachama mpya za Posta na za zamani zote
zitatumika. Jambo la kuzingatia ni kwamba lazima ziwe hai zimelipiwa ada na
mwanachama lazima awepo katika kitabu ch orodha ya wanachama wa klabu na tawi
lake,”amesema Mkwasa.
Ikumbukwe Yanga imekuwa chini ya Kaimu Mwenyekiti, Clement
Sanga kufuatia kujiuzulu kwa aliyekuwa Mwenyekiti, Yussuf Manji Mei mwaka jana.
Manji aliingia Yanga mwaka 2006 kama mdhamini kupitia
kampuni yake ya Lotto Kitita, lakini baadaye akawa mfadhili Mkuu wa klabu kabla
ya kuwa Mwenyekiti.
Katika kipindi chake cha kuwa mfadhili na Mwenyekiti wa
Yanga, Manji aliifanyia mengi klabu– kubwa ni kuirejeshea hadhi na heshima
klabu hiyo.
Alipoingia mwaka 2006 aliikuta klabu ipo dhoofu kiuchumi na
haiwezi kushindana na mahasimu wao, Simba katika kuwania wachezaji bora ambao
ndiyo mtaji wa kushinda mataji.
Wakati huo Yanga ilikuwa inasajili wachezaji ambao ama
walikuwa wameachwa na timu zao, waliojipeleka wenyewe kwa mapenzi yao au
waliopatikana kwa njia ya mchujo wa majaribio.
Lakini mara baada ya Manji kuingia Yanga, klabu hiyo ikaanza
kusifika kwa kusajili wachezaji wa kigeni na wale nyota wa hapa nyumbani, ikiwa
ni pamoja na kubomoa ngome ya mahasimu, Simba SC.
Mwaka 2009 fedha za Manji zilimtoa kipa kipenzi cha wana Simba
Msimbazi, Juma Kaseja na desturi hiyo ikaendelea baadaye wakichukuliwa beki
Kelvin Yondan na mshambuliaji Mganda Emmanuel Okwi.
Yanga iliipiku Simba ‘kimafia’ katika kumsajili beki
anayeweza kucheza kama kiungo pia, Mbuyu Twite kutoka APR ya Rwanda, tu kwa
jeuri ya fedha.
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Simba, Alhaj Ismail Aden Rage
alianza kuonekana akimsainisha Mbuyu mjini Kigali, lakini baadaye Mwenyekiti wa
Usajili wa timu ya Jangwani, Abdallah Bin Kleb akaingia kwa ‘gia kubwa’ na
kubadilisha mambo, Mbuyu akatua Jangwani.
Na ni katika kipindi hicho imeshuhudiwa Manji amewazima
kabisa Simba na Yanga ikitawala soka ya Tanzania na kuzidi kujiongezea
mashabiki na wapenzi.
Lakini migogoro haikukosekana pia wakati wa utawala wa
Manji, ambayo wakati fulani iliiathiri timu mfano ule wa kutaka kumng’oa
aliyekuwa Mwenyekiti, Wakili Lloyd Nchunga ulioiponza klabu ifungwe 5-0 na
mahasimu, Simba Mei 6, mwaka 2012.
Mapema mwaka jana, Manji alikuja na mpango wa kutaka
kujikodisha klabu kupitia kampuni aliyoisajili kwa jina la Yanga Yetu, lakini
ukapata upinzani mkali na kuamua kuachana nao.
Kabla ya kufikia maamuzi haya, Manji alipitia kwenye
misukosuko na Serikali kuanzia Januari hadi Aprili, kwanza akikamatwa na
kuwekwa ndani kwa tuhuma za kujihusisha na biashara.
Chanzo: Bin Zubeir
