Ugonjwa wa Ebola nchini Jamhuri ya Demokrasi ya Congo sasa umesambaa kutoka maeneo la vijijini hadi mji mmoja wa eneo hilo na kuzua hofu kuwa huenda sasa ikawa vigumu kuudhibiti ugonjwa huo.
Waziri wa afya Oly Ilunga Kalenga alithibitisha kisa cha ugonjwa huo mjini Mbandaka, mji wa wakaazi milioni moja ulio kilomita 130 kutoka eno ambapo kisa cha kwanza kilithitishwa mapema mwezi huu.
Mji huo ni muhumu kwa usafiri ukiwa na barabara zinazoelekea mji mkuu Kinshasa,
Kenya yachukua hatua baada ya Ebola kuripotiwa DR Congo
Watu 40 kwa sasa wameambukizwa na wengine 23 wanaripotiwa kufariki.
Ebola ni ugonjwa hatari ambao unasasabasha kufuja kwa damu ndani ya mwili na mara nyingi huua. Unaweza kusambaa kwa haraka kupitia kwa maji maji ya mwili na dalili zake hazitambuliwi kwa urahisi.
Mbona kusambaa kunaleta hofu?
Mlipukoam wa Ebola wa mwaka 2014-16 Afrika uliowaua watu 11,300 ulikuwa mbaya zaidi kwa sababu ulisamba kwenda miji mikuu ya nchi za Guinea, Sierra Leone na Liberia
Afisa wa cheo cha juu wa shirika la afya duniani (WHO) Peter Salama alisema kusambaa kwa ebola kwenda Mbandaka kunamaanisha kuwa huenda kukawa na visa vya milipuko ya ugonjwa huo.
map
Image caption
Ramani
Ni hatua gani inachukuliwa kudhibiti mlipuko huo?
Visa vilivyothibitishwa vya ugonjwa huo vimerekodiwa sehemun tatu kwenye mkoa wa Equateus, kwa mujibu wa WHO.
Wafanyakazi wa afya wametambua watu 430 ambao huenda wakikarbiana na ugonjwa huo na pia wanajaribu kuwatafuta wengine 4000 ambao wametawanyika kwenda kaskazini magharibi mwa Congo.
Ugonjwa wa Ebola wasambaa kwenda mji wa Mbandaka nchini DRC
Wengi wa watu hawa wako maeneo ambayo yanaweza kufikiwa na watu kwa kutumia pikipiki.
Siku ya Jumatano dawa ya majaribio ya ugonjwa wa ebola iliyotumwa na WHO iliwasili nchini humo huku nyingine ikitarajiwa kuwasili hivi karibuni,
Mbona ugonjwa wa Ebola unarejea mara kwa mara?
Kumekuwa na milipuko mitatu ya Ebola nchini DRC tangu janga la mwaka 2014-2016, Ebola inaaminiwa kusambazwa maeneo ya mbali na popo na mara nyingi husambaa kwenda kwa binadamu kupitia nyama ya msituni.
Watu 18 waambukizwa Ebola DRC
Pia unaweza kusambaa kwenda kwa binadamu kwa njia ya damu au viungo au majimaji ya mwili kutoka kwa wanyama walio ugonjwa huo. Hao ni pamoja na sokwe, tumbili na swara.
Ugonjwa huo husambaa kwa haraka na sio rahisi kumaliza wanyama wote wanaoweza kuwa nao. Ikiwa binadamu watakaribiana na wanyama hao kawaida kuna uwezekano kuwa Ebola unaweza kurudi.
