Mlinda mlango wa timu ya Juventus, Gianluigi Buffon ametangaza kustaafu soka katika klabu ya Juventus baada ya msimu kumalizika.
Buffon ambaye ni nahodha wa Juventus ameiongoza timu yake kushinda taji la Seria A mara saba, ikiwa pamoja na msimu huu ambapo timu hiyo inatwaa taji hilo kwa mara ya nne mfululizo.
Buffon ambaye hajawahi kushinda ligi ya mabingwa barani ulaya wakipoteza fainali tatu ameendelea kuweka rekodi ya kucheza dakika 974 (mechi 10) bila kuruhusu goli na kutwaa jumla ya mataji tisa.
Mabingwa hao wa Seria A watacheza dhidi ya Verona hapo kesho na utakuwa mchezo wa mwisho wa Buffon kwenye Ligi hiyo ya Seria A.
