Kiatu cha dhahabu cha Salah kukaa kwenye makumbusho England



Mshambuliaji wa timu ya Taifa ya Misri na klabu ya Liverpool, Mohammed Salah amepewa heshima nchini Uingereza katika makumbusho ya London.

Salah amepewa heshima hiyo kufuatia rekodi yake ya kuwa mfungaji wa muda wote aliyoiweka katika Ligi ya Premier nchini humo kwa mfano wa kiatu chake cha dhahabu kukaa katika makumbusho ya taifa hilo kwenye kumbukumbu za nchi ya  Misri.

Salah, ambaye ni mfungaji bora wa ligi hyo mwenye magoli 32, pia ameshinda tuzo ya mchezaji bora kwa Shirikisho la wacheza soka ya kulipwa mwaka 2017/18 (PFA).

Salah amefunga magoli  44 katika michezo 51 aliyocheza  msimu huu  hivyo anapata nafasi ya kuiongoza timu yake katika mchezo wa fainali wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Real Madrid mchezo utakaochezwa May 26 nchini Ukraine.

Post a Comment

Previous Post Next Post