Na Aminah Kasheibar, 24SevenUpdater.
Kushuka kwa soko la filamu nchi kumepelekea Nguli wa filamu za bongo movie, Jacob Steven 'JB' kutangaza kujiengua rasmi kwenye tasnia ya filamu nchini.
JB amesema anatarajia kustaafu kazi ya uigizaji rasmi na kufanya shughuli zake binafsi kutokana na ufinyu wa soko la filamu kwa sasa.
JB amesema kwasasa anajiandaa kumalizia tamthilia ya 'Kisasi cha moyo' sehemu ya pili baada ya hapo anamalizia fikamu ya mwisho ya Single Mother.
Amesema ameigiza kwa miaka mingi sana na kupata mafanikio makubwa na kujulilana ndani na nje nchi.
"kazi yangu ya Single Mother ndio itakuwa ya mwisho kuonekana katika televisheni ila nitakuwa nipo nyuma ya kamera kwaajili ya kuwaongoza waigizaji.
"kwasasa nawachia wasanii machipukizi ambao nimeamua kuwapa nafasi ili waweze kuonekana na kukuza vipaji vyao ili na wao waweze kufikia malengo yao, " amesema JB.
Hata hivyo JB amesema kushuka kwa soko la filamu wasanii hajachangia bali wasimamizi ndio chanzo kikubwa.
