Na Aminah Kasheibar, 24SevenUpdater
Warembo 20 wajitokeza kwenye usajili wa mashindano ya kumsaka mlibwende wa Miss Kinondoni.
Mratibu wa mashindano hayo, Rahma George amesema katika usajili huo wanaangalia vigezo muhimu ambavyo mlibwende anatakiwa kuwa navyo.
Alisema wameamua kufanya usajili huo wa wilaya ili kuwapa fursa warembo wenye vipaji kwasababu zamani kulikuwa na mashindano ya kitongoji lakini sasa hayapo tena.
"Tumeamua kufanya usajili huu wilaya ya kinondoni kwasababu ya kuwapa fursa warembo wenye vipaji ili waweze kufikia malengo yao pia mashindano haya yanamfanya binti kujielewa namna ya kuishi na jamii.
"Kwa wale ambao hawata chaguliwa kushiriki kwenye mashindano hayo wasikate tamaa zaidi ya kujiongeza kielimu na kujitolea katika jamii," alisema Rahma.
Rahma amesema baada ya mwezi wa Ramadhani ndio wataanza rasmi mashindano ya kumsaka mlibwende wa Miss Kinondoni.
Usajili huo uliofanyika Mei 13 mwaka huu katika ukumbi wa Millennium Tower Kijitonyama Dar es Salaam na kusimamiwa na kampuni ya Rahma internment na Miss atakayepatikana wilaya ya Kinondoni atashiriki katika kinyang'anyiro cha kumsaka Miss Dar es Salaam na baadaye Miss Tanzania.
