Filamu ya akina Ebitoke yawa gumzo Dar

Na Aminah Kasheibar, 24SevenUpdater

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Ally Hapi amewapongeza kampuni ya Timamu Movie kwenye uzinduzi wa trela la filamu ya 'Sema'.

Hapi amesema amefurahi kuona vijana wanafanya kazi mzuri katika kuelimisha jamii kupitia kazi wanazozifanya.

"Najivunia kuona vijana wanafanya kazii mzuri kwaajili ya kuelimisha jamii kwa maendeleo ya maisha yao ya baadae ukiona mtu amefanya kazi kwa muda mrefu harafu akaja kutoa watu mbalimbali basi huyo ni kiongozi bora," alisema Hapi.

Muandaaji wa timamu movie, Timoth Colado amesema lengo la filamu hiyo ni kutoa elimu kwa jamii na kukuza vipaji kwa vijana ili waweze kufikia malengo yao.

Amesema movie hiyo ni mwanzo na wataendelea kutoa kazi mzuri ili watangaze nchi ya Tanzania.
"Tumeamua kuzindua tera la movie hii kwaajili ya kubadilisha soko la filamu nchini kupitia kazi hii tutaweza kufikia Mbali.

"Katika filamu ya sema walioigiza ni ebitoke pamoja na bwana mjeshi kama wanzalishi na wengine mtawaona kwenye kazi zingine," amesema Timoth.

Hata hivyo timoth amesema baada ya Ramadhani ndio watazindua movie hiyo. Uzinduzi huo ulifanyika katika ukumbi wa Serena hoteli Posta Dar es Salaam, na Ally Hapi ndiye aliyekuwa mgeni rasmi.

Post a Comment

Previous Post Next Post