Ufafanuzi wa Kamishna Mkuu wa Magereza kuhusu kutoka kwa Sugu.


Kamishna Mkuu wa Magereza Kamishna Malewa ametoa ufafanuzi kuhusu kuchiwa huru kwa Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi 'Sugu' na Katibu wa Chadema Kanda ya Nyasa Emmanuel Masonga

"Ni kweli kwamba Joseph Mbilinyi alikuwa amepata kifungo cha miezi mitano, lakini Rais Magufuli katika kuazimisha siku ya muungano alitoa msamaha kwa wafungwa na sifa moja wapo ilikuwa aina ya kifungo alichonacho Sugu, kosa lake lilikuwa ni lugha ya matusi kutokana na sifa za kifungo hicho na ilikuwa moja ya sifa ni awe ametumikia robo ya kifungo chake iliruhusiwa atoke tarehe 10 mwezi Mei ambayo ni leo na hii inatokana na msamaha kutoka kwa mh rais.

"Si kweli kwamba ilikuwa atoke kesho na hili la kutoka mlango wa nyuma si la kweli kwasababu gereza lina mlango mmoja tu hakuna lenye milango miwili". Muda huu

Post a Comment

Previous Post Next Post