Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, amethibitisha kuwa Mbunge wa Mbeya mjini Joseph Mbilinyi 'Sugu'na Katibu wa Chadema kanda ya Nyasa Emmanuel Masonga wameachiwa huru asubuhi hiii
Mbowe amewasili majira ya saa 12 asubuhi akiongoza msafara wa wa mapokezi wa viongozi hao kwenye gereza la Ruanda walilokuwa wamfungwa akiwa sambamba na mbunge wa Viti Maalumu, Sophia Mwakagenda na viongozi wengine wa chama hicho
Viongozi wengine waliofika garezani hapo ni pamoja na Meya wa Jiji la Mbeya, Mchungaji David Mwashilindi na madiwani.
Askari wamefika gereza kuu kuimarisha ulinzi wakiwa na magari mawili, moja limeingia ndani na lingine lipo nje.
Sugu na Masonga walitiwa hatiani na kuhukumiwa kifungo cha miezi mitano jela Februari 26 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya kwa kutoa lugha ya fedheha dhidi ya Rais John Magufuli kwenye mkutano wa hadhara walioufanya Desemba 30 mwaka jana eneo la Shule ya Msingi Mwenge jijini Mbeya.
Wawili hao wameshatumikia adhabu hiyo kwa siku 73 ikiwa ni zaidi ya robo ya kifungo chao.
