Paroko Msaidizi wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Yosefu katika
Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Venance Tegete amefariki dunia jioni ya leo Mei 26,
2018 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili aliko lazwa kwa ajili ya matibabu
kabla ya kufikwa na umauti.
Taarifa ya kifo cha marehemu Padre Tegete imethibitishwa na Askofu
Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo.
Katibu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Pd. Frank Mtavangu
amesema taratibu za mazishi zinafanywa na kwamba taarifa zaidi zitatolewa
baadae.
