Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job
Ndugai amemlilia Mbunge wa jimbo la Buyungu (Chadema) kutoka mkoani Kigoma,
Kasuku Samson Bilago aliyefariki dunia mchana wa leo katika Hospitali ya Taifa
Muhimbili.
Kupitia taarifa yake aliyoitoa kwa umma leo Mei 26, 2018,
Spika Ndugai amesema ofisi ya bunge inaendelea kuratibu taratibu za mazishi kwa
kushiriukiana na familia ya marehemu Bilago.
Taarifa hiyo imeeleza kwamba mwili wa Bilago unatarajiwa
kuagwa bungeni siku ya Jumatatu ya Mei 28, 2018 na baadae kupelekwa Kankonko
mkoani Kigoma kwa ajili ya mazishi.
Awali marehemu Bilago alilazwa katika hospitali ya DCMC
iliyoko jijini Dodoma ambapo baadae alihamishiwa Muhimbili alikofikwa na
umauti.
