Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amemteua Khadija
Issa Said kuwa Naibu Kamishna wa Mamlaka ya Kusimamia Shughuli za Bima nchini-TIRA
.
Taarifa hiyo imetolewa leo na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya
Rais Ikulu, Gerson Msigwa.
Taarifa hiyo inaeleza kuwa, kabla ya uteuzi huo Khadija Issa
Said alikuwa Mkurugenzi wa Idara ya Bima, Shirika la Bima Zanzibar.
“Uteuzi wa Bi. Khadija Issa Said umeanza leo terehe 26 Mei,
2018,” inaeleza sehemu ya taarifa hiyo.
