Watu Takribani 22 wakiwemo watoto watatu wameuawa kwenye
ajali ya basi nchini Uganda.
Ajali hiyo ilitokea jana usiku
maeneo ya Kiryandongo karibu kilomita 220 kaskazini mwa mji mkuu wa Uganda, Kampala.
Taarifa hiyo imetolewa na Msemaji wa jeshi la polisi nchini
Uganda, Emilian Kayima kupitia mtandao
wa AFP.
Kayima amesema basi hilo liligonga tingatinga ambayo ilikuwa
ikiendeshwa bila ya taa.
