Nyota wa Msimbazi Shiza Kichuya ameweka wazi kuwa sasa ni muda muafaka wa yeye kutimka kwenye klabu yake na kwenda kwenye kucheza mpira majuu.
Wakati huo huo klabu hiyo imefanikiwa kuinasa saini Straika wa klabu ya Majimaji Marcel Boniventure kiheza na kutua rasmi kwenye klabu hiyo.
Taarifa kutoka ndani ya Klabu hiyo bingwa zimelea kuwa Kiheza alisafiri Alhamisi kutoka Songea na kutinga Dar es Salaam kwa ajili ya kuungana na mabingwa hao wa VPL.

Kichuya anasema amesikia maoni ya baba yake mzazi akimtaka kuondoka kwenda nje kucheza soka la kulipwa na lenye masilahi zaidi na amesema analifanyia kazi kwa nguvu zote.
“Najua hilo limekuwa likimuumiza lakini hata mimi napambana kufanya vizuri ili niweze kupata nafasi ya kwenda kucheza nje na hilo ndiyo lengo kubwa la kujituma kwa sababu nataka kuondoka hapa nilipo na wakati wowote kutoka sasa iwapo mipango yangu itafanikiwa kwenda vizuri,” alisema Kichuya.
Kichuya amesema yupo tayari kuondoka kwenye timu hiyo mwishoni mwa msimu huu iwapo mambo yake yatakwenda vizuri.
Kichuya alijiunga na Simba msimu uliopita kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Mtibwa Sugar huku akiripotiwa kupokea mshahara wa Sh Mil 1.8 katika kikosi cha Simba licha ya kuwa ni mchezaji muhimu kikosini humo.
“Suala la mkataba mpya na Simba siwezi kuliongelea kwa sababu bado sijamaliza mkataba wa kwanza hadi hapo utakapokwisha nitaweka wazi, kweli baba yangu amesema nikacheze nje ni sawa kwa sababu ni maoni yake kama mzazi maana anaona akina Simon Msuva, Mbwana Samatta na Abdi Banda wakifanya vizuri nje.