Jeshi la Kujenga Taifa-JKT imetaja orodha ya majina ya
waliohitimu kidato cha sita walioteuliwa kujiunga na mafunzo mbalimbali ikiwemo uzalendo, umoja wa
kitaifa, stadi za kazi na maisha kwa ajili ya kulitumikia taifa.
Taarifa hiyo imetolewa leo kwa umma na JKT, ambapo imetaja
tovuti yenye orodha kamili ya majina ya vijana walioteuliwa na makambi ya JKT
waliyopangiwa, ambayo ni www.jkt.go.tz
Sehemu ya taarifa hiyo inaeleza kuwa, walioteuliwa watatakiwa
kujigharamia nauli za kwenda na kurudi kwenye makambi ya JKT waliyopangiwa
wakiwa na vifaa mbalimbali.
Vile vile JKT limewapangia kambi watu wenye ulemavu wa
kuonekana kwa macho, ambayo imetajwa kuwa Ruvu JKT iliyoko mkoani Pwani ambako ina
miundombinu ya kuhudumia jamii hiyo.
