Korea Kaskazini imekubali kuondoa silaha za nyuklia katika
rasi ya Korea pamoja na kuhudhuria mkutano wa kukutana na Rais wa Marekani,
Donald Trump unaotarajia kufanyika Juni 12, 2018 Singapore.
Taarifa hiyo imethibitishwa na Rais wa Korea Kusini, Moon
Jae-in baada ya kufanya kikao jana Jumamosi na Rais wa Korea Kaskazini, Kim
Jong-un.
Mkutano huo kati ya viongozi wa Korea kaskazini na Korea Kusini
ni mabadiliko ya hivi karibuni, katika wiki iliyogubikwa na misukosuko ya
kidiplomasia kuhusiana na mkutano wa kilele wa aina yake ambao haukuwahi
kutokea kati ya Marekani na Korea Kaskazini.
Chanzo: D.W Swahili
