Mwenyekiti wa Kamati Maalumu ya Kuhakiki mali za CCM
iliyoundwa na mwenyekiti wake Rais John
Magufuli, Dkt. Bashiru Ally ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa chama hicho.
Dkt. Bashiru ambaye ni Mwalimu Mwandamizi kutoka Chuo Kikuu
cha Dar es Salaam, ameteuliwa na wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM- NEC
kuurithi wadhifa huo uliokuwa chini ya Abdulrahman Kinana kabla ya kujuzulu
hivi karibuni.
Wajumbe wa NEC walimteua Dkt. Bashiru kuwa Katibu Mkuu wa
CCM katika Mkutano wake uliofanyika leo kwenye Ukumbi wa Kikwete ulioko Ikulu
Jijini Dar es Salaam.

