Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Vijana chini ya miaka 20 (Ngorongoro Heroes) Ammy Ninje ameahidi ushindi katika mchezo wao wa raundi ya pili kufuzu fainali za Afrika kwa Vijana dhidi ya Mali, mchezo utakaochezwa Jumapili Mei 13, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Ninje amesema anafahamu vyema kuwa Mali ni timu nzuri na amekuwa akiifuatilia kwa karibu, lakini kwa upande wa Ngorongoro Heroes wao wamejiandaa vizuri kuhakikisha wanafanya vema katika mchezo huo
Naye Nahodha wa Ngongoro Heroes, Issa Makamba amesema kikosi chao kipo tayari kwa mapambano na wanaamini watashinda.
Watanzania wanatakiwa kujitokezaa kwa wingi katika uwanja wa taifa, kuwashangilia Ngorongoro Heroes, mchezo utakaoanza majira ya saa 10 alasiri, kiingilio katika mchezo huo ni Sh. 3,000 kwa VIP na Sh. 1,000 kwa viti vya mzunguko.
