Dani Alves kulikosa Kombe la Dunia


Timu ya Taifa ya Brazil imepata pigo baada ya beki wake wa kulia, Dani Alves kupata jeraha la goti na kumpelekea kukosa mashindano ya Kombe la Dunia 2018.

Alves (35) atakosa mashindano hayo baada ya kupata jeraha katika goti lake la kulia kwenye kombe la Ufaransa akiwa na timu yake ya PSG dhidi ya Les Herbiers wiki hii. 

Beki huyo wa zamani wa Barcelona na Juventus ameshinda jumla ya mechi 106 na msimu huu amechezea PSG michezo 41 na kuisaidia kutwaa taji, pia alicheza mwaka 2010 na 2014 katika mashindano ya Kombe la Dunia. 

Mabingwa wa dunia mara tano Brazil wapo kundi E pamoja na  Uswisi, Costa Rica na Serbia.

Post a Comment

Previous Post Next Post