Simu ya Nondo yaibuliwa Mahakamani



Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoa wa Iringa imeendelela kusikiliza ushahidi katika kesi inayomkabili Mwenyekiti wa Mtandao wa wanafunzi (TSNP) nchi Abdul Nondo ambapo shahidi amedai mahakamani kuwa simu ya Nondo ilikuwa kitumika wakati aliodaiwa kutekwa.
Shahidi huyo ambaye ni Ofisa wa Jeshi la Polisi kwenye kitengo cha Makosa ya mtandaoni Abdul Kareem.

Shahidi huyo alidai kuwa hakuweza kujua simu ya Nondo ilikuwa ikitumiwa na nani kutokana na yeye hana uwezo kutambua ni nani alikiwa akiitumia.

 Wakili Jebra Kambole amesema kwamba mbali na Shahidi Abdul Kareem, Koplo John ambaye ni mpelelezi katika kesi hiyo ametoa ushahidi wake ambao ni maelezo ya Nondo aliyoyatoa katika kituo cha polisi Iringa.
Wakili Kambole amesema kwamba licha ya serikali kuwa na mashahidi watano katika kesi hiyo, Juni 12-13 inategemea kuwepo na mashahidi wengine ambao bado hawajajulikana watakuwa wangapi.
Hakimu katika kesi hiyo John Mpitanjia ameahirisha kesi hiyo mpaka Juni 12 ambapo Mtuhumiwa Abdul Nondo ataendelea kuwa nje kwa dhamana.
Nondo anatuhumiwa kwa makosa mawili Kosa la kwanza ni kuchapisha taarifa za uongo mtandaoni Machi 7, 2018 akiwa Ubungo na kusambaza kwa kutumia mtandao wa WhatsApp kuwa yupo hatarini, kosa la pili ni kutoa taarifa za uongo akiwa mjini Mafinga kwa askari Polisi wa kituo cha Mafinga Wilayani Mufindi.

Post a Comment

Previous Post Next Post