Upo usemi unaosema mazoea yanatabu ndivyo inavyothibiti kwa Mkali wa Bongo Flavor Nasibu Abdul (Diamond Platnum) baada ya kushindwa kuvumilia kuishi mbali na mzazi mwenza wake Zari.
Updater imejuzwa kuwa Diamond hayupo tayari kuishi mbali na watoto wake waliozaa pamoja na Zari Tiffa na Riaz. Anachukizwa na kitendo cha watoto wake kukosa malezi yake.
Diamond amekiri kwenda kwa Zari nchini Afrika Kusini mara mbili akidai ameenda kwa ajili ya watoto wake na kwamba isingependeza yeye kuishia kutuma pesa bila kwenda kuwaona watoto wake.
Hata hivyo Mgororo ulibuka kati wawili hawa ulimalizwa kwa kuachana ambapo Zari ndiye aliyetangaza kuachana na Diamond .
Washikaji wa karibu wa Diamond wanasema kuwa rafiki yao kwa sasa anaonekana kuyumba ingawa sio kwa uwazi "anaonekana kuwa hayupo sawa".
Diamond hajaweka wazi na amekanusha kuomba msamaha lakini haitakuwa jambo la kustaajabisha tena ikiwa Diamond akionekana wamerudiana na Zari.

