Uchawi wa Yanga ni huu -Rage


Aliyekuwa mwenyekiti wa klabu ya Simba, Ismail Aden Rage, amesema kuwa sababu ya watani wao  wa jadi Yanga kushindwa kufanya vizuri msimu huu katika Ligi Kuu Bara sio ukata wa  fedha.

Amesema kuwa tatizo la Yanga ni ukata wa wachezaji wazuri ambapo wengine wenye viwango ni majeruhi



Rage amesema Yanga walipaswa kuwafanyia vipimo vya afya wachezaji wao ili kuweza kujua kama wapo fiti kuweza kutumika katika mashindano mbalimbali ikiwemo ya kimataifa.

"Pesa si sababu iliyosababisha Yanga kufikia hatua waliyonayo hivi sasa kwasababu wanapata kutoka kwa mdhamini ambaye pia anatoa mpunga wake kwa Simba ambaye ni SportPesa".

Ametoa ushauri  timu zingine kufanya vipimo vya afya kwa wachezaji wanaowasajili ili kuepuka matatizo kama ambayo Yanga wameyapata kwenye msimu huu.

Post a Comment

Previous Post Next Post