Klabu ya Simba imendelea kuzinasa mashine za magoli baada ya kukamilisha taratibu za usajili kwa mtia kimyani wa Klabu Lipuli FC ya Iringa, Adam Salamba na kuwaacha Solomba watani wao wa jadi klabu ya yanga iliyokuwa ikimtaka.
Mabingwa hao wapya wa ligi kuu Bara wamejihakikishia kumnasa mshambuliaji huyo baadsa ya kuwazidi kete watani wao wa jadi kwa ajili ya kumtumia kwenye hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Awali yanga waliwahi kupeleka barua Lipuli kabla ya Simba ya kumuomba mshambuliaji huyo ili wamtumie kwenye mi¬chuano hiyo ya kimataifa na kujibiwa kanuni zinawazuia Salamba kutua Yanga kuto¬kana na kuzichezea timu mbili katika msimu mmoja, Stand United na Lipuli.
Taarifa ndani ya Klabu ya Simba zinasema kuwa kwa Salamba kilichobakia ni kusaini ili aanze kukipiga ndani klabu hiyo.
