Na
Aminah Kasheiba, 24SevenUpdater
Msanii wa filamu za Bongo Movie, Steve Nyerere
amesema wasanii wanatakiwa kuwa na ushirikiano katika vipindi vya dhiki na
faraja ili waweze kufika mbali kisanaa.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es
Salaam Steve ametolea mfano msiba wa Masogange na kusema kuwa wasanii walishirikiana
kwa muda wote hivyo ushirikiano huo uendelee kwani hakuna anaejua kesho.
“Tunapaswa kushikamana kwa kipindi chote kwani
ushirikiano ndio unasaidia hata kazi zetu za sanaa kufika mbali majungu na
fitina hazina msingi wowote ule.
“Sote ni kitu kimoja hivyo tunatakiwa kushikana na
kuwa mfano kwa jamii ukizingatia sisi ni kioo cha jamii,’’ amesema Steve.
