Nyota wa muziki wa bongo fleva, Nassib Abdul
‘Diamond Platinum’ anatarajia kushiriki kwenye uzinduzi wa Kombe la Dunia
nchini Urusi.
Kombe la Dunia linatarajiwa kuanza mwezi , Juni
mwaka huu ambapo Diamond atakuwa Balozi akiwakilisha wasanii wengine kutoka
Tanzania.
Baadhi ya wasanii wanaoungana na Diamond Plantinum
katika uzinduzi huo ni Jason Deruro, Cassper Nyovest na waimbaji wengine kutoka
nchi mbalimbali za Afrika kama Uganda, Ethiopia na Msumbiji ambao wataimba
wimbo wa pamoja unaoitwa ‘Color’.
Diamond amesema amefurahi kupata fursa ya kushiriki
kwenye uzinduzi huo na kuwa mmoja wa wasanii kutoka Tanzania.


Amesema kuwa nafasi aliyoipata atatuimia vizuri kwa
lengo la kukuza soko la muziki wa Tanzania na kuitangaza nchi kupitia fursa
hiyo.
“Nimefurahi kupata nafasi hii kwani inanipa nguvu
ya kufanya kazi kwa bidii zaidi kwani fursa niliyoipata ni ya kipekee na
nitaitumia vizuri.
“Wimbo wa ‘Color’ nitakaouimba kama remix ambao
siku hiyo ndio nitaimba kwa lengo la kuitangaza tamaduni ya Tanzania ili watu
wajue,’’ amesema Diamond.
Hata hivyo Diamond amesema wimbo huo wa ‘Color’ umeandaliwa
na Emmanuel Mkono ‘Nahreel’.
