Mke wa aliyekuwa rais wa Marekani George HW Bush afariki


Mke wa aliyekuwa rais wa zamani wa Marekani George HW Bush, Barbara Bush amefariki akiwa na umri wa miaka 92.
Barbara ndiye aliyekuwa nguzo ya kisiasa ya marais wawili wa taifa hilo akiwemo mumewe George HW Bush na mwanawe George W Bush.
Bi Bush ambaye alikuwa mke wa rais toka 1989 hadi 1993 amekuwa afya yake imekuwa ikidorora kwa muda sasa na alikuwa amekataa kupatiwa matibabu zaidi.
Risala za rambirambi zimetumwa nchini Marekani kutoka maeneo tofauti duniani.
Mke huyo wa rais wa zamani, mumewe ambaye ana umri wa miaka 93 ndiye rais aliyeishi kwa muda mrefu nchini Marekani.

Barbara Bush na mumewe aliyekuwa rais wa Marekani George HW Bush
Image captionBarbara Bush na mumewe aliyekuwa rais wa Marekani George HW Bush

Mwana wao George alichaguliwa 2000 na kuhudumu kwa miula miwili kama rais wa 43 wa Marekani.
Katika tanzia alisema katika taarifa yake kwamba ''mamangu mpendwa ametuwacha akiwa na umri wa miaka 92. Laura Barbara, Jenna na mimi tunaomboleza , lakini roho zetu zimepumzika kwa sababu tunajua yake pia imepumzika.

Post a Comment

Previous Post Next Post