Na Abdul Hussein, 24SevenUpdater
Kwa hali isiyo ya kawaida jana mtangazani wa Clouds Fm Diva maarufu kama Divetheabawse amemshushia mvua ya matusi aliyekuwa mtangazaji mwenzake Michael Lukindo maarufu kama MR Infoma
Lukindo ambaye kwa sasa amejikita kwenye uimbaji wa muziki wa kizazi kipya alijikuta katika wakati mgumu alipo kuwa anatambulisha wimbo wake mpya wa "Basi iwe" wiki iliyopita ndipo alipo ulizwa na mmoja wa watangazaji wa Cloud Fm Mamy Baby juu ya uhusiano wake yeye na Diva
Lukindo hakuweza kuweka wazi moja kwa moja kuhusu mahusiano yao na mwana Dada huyo bali alibaki kujikanyaga kanganya juu ya swali hilo
Hata hivyo Mwana dada huyo hakuweza kusema chochoti kuhusiana na tuhuma hizo za kutoka kimapenzi na Lukindo
Kupitia kipindi cha XXL jana kwenye kipengele cha Shilawadu kinachoongozwa na Soudy Brown, Lukindo alikili kutoka kimapenzi na Mwana dada huyo ambapo Soudy aliwaunganisha wawili hao kupitia simu ya Ndipo Diva alimshushia matusi Lukindo na kudai kuwa atamshitaki kwa kosa la "defamation"(kashifa).
