Watalii waikimbia Hoteli kwa kuchapwa bakora na Mashetani


'Ukistaajabu ya Musa, utayaona ya Firauni ' usemi huu umejidhiwhirisha Kisiwani Mafia Kwenye kijiji cha Bweni ambako Hoteli ya Kitalii imetelekezwa kwa sababu ya wageni na wamiliki wa hoteli hiyo kushindwa kukaa kutokana na kuchapwa na bakora  bila kumuona anayewachapa wakati wa Usiku.

Hoteli hiyo iliyotajwa kumilikiwa na Raia wa kigeni aliyefahamika kwa jina la Peter iliyokuwa kwenye fukwe za pwani ya Bweni Kaskazini mwa kisiwa hicho.

Wageni wanadaiwa kuchapwa na Bakora nyakati za usiku wakiwa wamelala bila kuona anayewachapa wala kuona zinapotokea bakola hizo badala yake kuugulia maumivu ya kuchapwa.



Baadhi ya maeneo ya Hoteli hiyo
24SevenUpadater ilielezwa na Mwenyeji wa Kijiji hicho Mwalimu Abdallah ambaye alisema kuwa upo uwezekano kuwa wageni hao wamepigwa bakora hizo na Mashetani "Hapa wazungu walikuwa wakifanya mambo ambayo yapo kinyume na maadili "

24SevenUpadater ilijionea majengo ya Hoteli hiyo yaliyotelekezwa bila kuwepo na mtu yoyote eneo hilo.


Post a Comment

Previous Post Next Post