Rais John Magufuli leo Aprili 23, 2018 amefanya uteuzi katika Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya Posta (TPB) ambapo amemteua Dk. Edmund Bernard Mndolwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi hiyo.
Mndolwa ambaye aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya KCB Tanzania pia alikuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya 'National Insurance Corporation' (NIC) anachukua nafasi ya Lettice Rutashobya ambaye amemaliza muda wake.
