Ronaldo aichafua rekodi yake


Usiku wa kuamkia leo Aprili 26 mchezo wa nusu fainali ya pili ya UEFA Champions League kati ya FC Bayern Munich kutoka nchini Ujerumani dhidi ya Real Madrid ya Hispania umechezwa.
Mchezo huo uliochezwa katika uwanja wa Allianz Arena ukiwa ndio mchezo wa kwanza ambapo baadae Bayern watacheza mchezo wa marudiano Santiago Bernabeu.
Katika mchezo huo Real Madrid wamefanikiwa kupata ushindi wa magoli 2-1 wakiwa ugenini dhidi ya FC Bayern ambapo magoli ya Real Madrid yalifungwa na Marcelo dakika ya 44 na Asensio dakika ya 57, Bayern Munich ndio wa kwanza kufunga goli dakika ya 28 kupita kwa Joshua Kimmich.

Hata hivyo rekodi ya Kimmich imevunjwa kwakuwa hakuna mchezo wa Bayern ya Champions League aliyowahi kufunga goli halafu wakapoteza, wameshinda michezo 10 na kutoka sare katika michezo miwili.




Hata hivyo staa wa Real Madrid Cristiano Ronaldo ameharibu rekodi yake katika michuano ya UEFA Champions League msimu wa 2017/2018, kwani mchezo huo uliochezwa usiku wa Aprili 25 ndio mchezo wake wa kwanza msimu huu kucheza bila kufunga wakati mwenzake Marcelo amefanikiwa kuendeleza rekodi yake, Real Madrid wamefunga mechi 32 kati ya game 33 ambazo Marcelo amewahi kufunga za mashindano yote.

Post a Comment

Previous Post Next Post