"Trump hashauriki" - James Comey


Aliyekuwa mkuu wa FBI nchini Marekani, James Comey amesema kuwa haamini kama kuna kiongozi yoyote wa karibu na Rais wa nchi hiyo, Donald Trump anaweza kumbadilisha tabia.

Comey amesema kuwa tabia zake zinahatarisha hadhi ya nchi.

Kabla ya kufukza na Trump, Comey aliongoza uchunguzi dhidi ya kuhusika kwa Urusi katika uchaguzi wa Marekani.

Akizungumza katika kipindi cha Newsnight Comey amesema tabia za Trump zinaathiri wale wanaomzunguka.

"Nadhani tabia yake inaathiri hasa kwenye suala la ukweli na jambo la msingi ni jinsi tabia hizo zinavyoathiri taasisi na watu wa karibu yake. Ana tabia ya kuongea uongo na kuwa lazimisha wale wanaomuunga mkono kukubaliana naye na kumuamini"



Trump alimshutumu Comey kuwa anayoyazungumza ni uongo na siasa zake za ubaguzi.

Haya yameanza wakati wa uchaguzi wa urais mnamo 2016, wakati Comey akiwa Mkurugenzi wa FBI na uchunguzi kuhusu namna mgombea wa urais wa chama cha Democrat Hillary Clinton alivyozishughulikia barua pepe za siri katika kompyuta binafsi wakati akiwa waziri wa mambo ya nje.

Mnamo Julai 2016, Comey alisema kwamba hakuwa na umakini katika namna alivyozishughulikia barua pepe hizo, lakini FBI haitomshtaki.

Hatahivyo mnamo Oktoba, sikukadhaa kabla ya uchaguzi, alituma barua bungeni akiliarifu kwamba FBI linaanzisha upya uchunguzi baada ya kugundua barua pepe zaidi.

Barua hiyo ilifichuliwa kwa umma na Hillary Clinton akasema hatua hiyo ndiyo iliompa Trump ushindi.

Mnamo November, FBI lilisema limekamilisha ukaguzi wa barua pepe hizo mpya zilizogunduliwa na kwa mara nyingine likasema halitomshtaki.

Na bwana Trump alipopata urais, Bwana Comey alisema kuwa alijaribu kumshurutisha aape kumtii - Jambo ambalo rais analikana pakubwa.

Mnamo Machi 2017, wakati uchunguzi ulipokuwa unafanywa na FBI kuhusu tuhuma za ushirikiano kati ya timu ya kampeni ya Trump na Urusi inatuhumiwa kwamba Trump alimshinikiza Comey kutangaza wazi kwamba rais hatochunguzwa kibinafsi - jambo ambalo mkurugenzi huyo wa zamani wa FBI alikataa kufanya hivyo.

Baadhi ya wanasiasa wa Democrats walimlaumu Comey kwa kumfanya Bi Clinton apoteze kura katika uchaguzi , huku wafuasi wa Trump walihisi kwamba anamlenga rais katika uchunguzi huo.

Alifutwa kazi na rais Trump mwezi Mei, na alipata taarifa kuhusu kutimuliwa kwake katika vyombo vya habari nchini.

Comey alihojiwa bungeni kuhusu uchunguzi huo wa uwezekano kuwepo uhusiano kati ya kampeni ya Trump na Urusi na kutimuliwa kwake, na alimthumu rais kwa kusema urongo na kumchafulia jina.

Orodha ya maafisa wa serikali ya Marekani waliofutwa kazi na rais Donald Traump tangu achukue mamlaka.

Rex Tillerson, waziri wa maswala ya kigeni - 13 Machi 2018

Gary Cohn, Afisa mkuu wa masuala ya kiuchumi - 6 Machi 2018

Hope Hicks, Mkurugenzi wa mawasiliano Ikulu ya Whitehouse - 28 Februari 2018

Rob Porter, Katibu katika Ikuku ya White House- 8 Februari 2018

Andrew McCabe, Naibu mkurugenzi shirika la FBI - 29 Januari 2018

Tom Price, Waziri wa afya - 29 Septemba 2017

Steve Bannon, Afisa mkuu wa mipango - 18 Agosti 2017

Anthony Scaramucci, Mkurugenzi wa mawasiliano - 31 Julai 2017

Reince Priebus, Afisa mkuu wa wafanyikazi wa umma - 28 Julai 2017

Sean Spicer, Waziri wa habari - 21 Julai 2017

James Comey, Mkurugenzi wa shirika la FBI - 9 Mei 2017

Michael Flynn, Mshauri wa maswala ya usalama - 14 Februari 2017

Sally Yates, Kaimu Mwanasheria Mkuu - 31 Januari 2017

Preet Bharara, Mwendesha Mashtaka wa New York federal prosecutor - 11 Machi 2017

Paul Manafort, Meneja wa Kampeni wa Trump - 19 Agosti 2016

Post a Comment

Previous Post Next Post