Baada ya kocha wa Arsenal , Arsene Wenger kukubali kuondoka kwenye klabu hiyo mwishoni mwa msimu huu, nguli wa zamani wa Arsenal, Patrick Vieira
anatarajiwa kurejea klabuni hapo na kuchukua mikoba ya Mzee Wenger.
Nahodha huyo wa zamani wa
timu hiyo na Ufaransa, anahusishwa na mpango huo kuchukua nafasi ya Wenger, baada ya wenger
kukiri kuondoka klabuni hapo mwishoni mwa msimu huu.
Taarifa zinaeleza kuwa Wenger amesalia Arsenal akiwa ni mmoja wa kiongozi
watakaokuwa katika benchi la ufundi.

