Video queen wa Bongo flavour wa muda mrefu Agness Gerald maarufu kama Agness Masogange amefariki dunia leo katika Hospitali ya Mama Ngoma, Mwenge jijini Dar es Salaam.
Akithibitisha taarifa ya kifo hicho, Muigizaji Steve Nyerere amesema kuwa Agnes amefariki kwa presha na mwili umepelekwa katika hospitali ya Muhimbili kwa uchunguzi zaidi.
Agnes Masogange alikuwa maarufu baada ya kuonekana kwenye video kadhaa za bongo ikiwemo Masogange ya Belle 9.
