Mabinti wawili Dorcas Atsea na Deborah Atoh raia wa Nigeria ambao walikuwa wanafunzi wa Mawasiliano ya Umma katika Chuo Kikuu cha Benue wamejikuta wakifanya mitihani wa mwisho wakiwa wamevalia mashela.
Kitendo hicho kimepelekea Mabibi harusi hao kushangaza watu huku ikielezwa kuwa hiyo ilitokea baada ya mabinti hao wate kupanga tarehe ya harusi ndani ya siku ambayo imepangwa kufanyika kwa mtihani ambao ulikuwa ufanyike mwezi February na ukaahirishwa na kupangwa siku ambayo iliangukia tarehe ya mabinti hao na familia zao walipanga iwe siku ya harusi.
Hata hivyo wawili hao iliwabidi wafunge ndoa na kukimbia chuoni ili kufanya mtihani huo na baadaye kwenda kuendelea na sherehe ya harusi.
Mabibi harusi hao walikuwa wanafunzi wa Mawasiliano ya Umma na walikuwa wanafanya mtihani wa somo la “Media Ethics and Law”.
Tags:
Mchanganyiko
