Mwakibinga awavaa Maaskofu KKKT


WARAKA wa wachungaji wa kanisa la kiinjili la kilutheri Tanzania KKKT  umeanza kupingwa kwa hoja  ya kuwa umeushambulia serikali zaidi,
Philipo Mwakibinga Mkurugenzi wa Utafiti  wa  Watetezi wa Rasilimali wasio na mipaka (Walami), akizungumza na vyombo vya habari leo amesema kuwa waraka wa maaskofu hao umeelemea kuikosoa serikali ambaopo wangeweza kuzungumzia masuala yao yahusiayo dini yao.
“Tunatoa wito kwa Maaskofu wetu kujikita katika masuala mahsusi yanayohusu Dini, watuelimishe kwenye dini, wamuachie Kaisari yaliyo yake  na Mungu yaliyo yake
“Tunashangaa ni kwanini waraka huu wa salamu za Pasaka  haukujikita zaidi katika kuwasisitiza waumini wake kujikita katika kuabudu, kumnyenyekea Mungu, kusoma bibilia na maandiko mengine ya dini na badala yake wakajikita katika maoni yanayong’ata na kupuliza” amesema.
Msemaji huyo ameshangazwa na viongozi hao kuzungumzia suala la katiba mya ilhali viongozi wa upinzani waliwahi kugoma kwenye bunge la kujadili rasimu ya Katiba mpya.
“Sote ni mashahidi kuwa Kuilazimisha Serikali kuitisha mchakato upya wa katiba ni jambo ambalo haliingii akilini kwa sasa kutokana na ukweli kwamba ni wanasiasa wenyewe hususan wa vyama vya upinzani ndio waliosusia na kukwamisha mchakato wa katiba kwa kutaka kulazimisha mawazo yao yawe bila kuzingatia msingi mama wa Demokrasia kuwa wachache wanasikilizwa wengi wanashinda” amesema.
Mwakibinga amesema kuwa anatilia shaka waraka huo kuwa unamikino ya kisisasa kutoka madai ya kusambazwa na Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema.
“Kwanini waraka huu wa Maaskofu umesambazwa kwa mara ya kwanza na kiongozi wa CHADEMA ambaye pia ni mjumbe wa kamati kuu wa chama hicho mheshimiwa Lema  ambaye ndiye aliusambaza Waraka wa Mbowe katika muda unaofanana na njia zinazofanana”

Post a Comment

Previous Post Next Post