Wakati Naibu Katibu Mkuu (Bara), John Mnyika na Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Serengeti, John Heche wakizuiliwa polisi kwa kushindwa kufuata taratibu za dhamana, Jeshi la Polisi limetoa amri ya kukamatwa kwa Mbunge wa Kawe, Halima Mdee na Ester Matiko.
Mdee na Matiko hawajafika kituoni hapo kutokana na kinachoelezwa kuwa ni kupata dharura.
“Mdee yupo nje ya nchi kwa matibabu na Ester Matiko yuko Dodoma kwa shughuli za kibunge amechelewa usafiri,” amesema Dk. Mashinji.
Walioachiwa kwa dhamana ni Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe, Naibu Katibu Mkuu (Zanzibar), Salum Mwalimu na Dk. Vicent Mashinji.
Heche na Mnyika hawakuripoti polisi Machi 16, 2018 huku chama hicho kikieleza kuwa moja ya sababu ya wabunge hao kutoripoti ni kutokana na kuhudhuria vikao vya kamati za Bunge mjini Dodoma.
