Rose Muhando kuibuka upya baada ya miaka 5

Muimbaji wa nyimbo za Injili Tanzania Rose Muhando alikuwa kimya kwa zaidi ya miaka mitano sasa bila ya kutoa album yoyote tofauti na miaka ya nyuma, kitu ambacho kilipelekea mashabiki wake kumiss album ya nyimbo zake baada ya kimya hicho.
Rose Muhando baada ya kimya hicho imetangazwa siku atakayoachia album yake mpya ya nyimbo za injili, Rose Muhando sasa ni rasmi ataitambulisha album yake April 1 siku ya tamasha la Pasaka jijini Mwanza na April 2 Simiyu.
Waandaaji wa tamasha la Pasaka linalofanyika mara moja kwa mwaka Alex Msamaamethibitisha maamuzi hayo ya Rose Muhando kuzindua album hiyo na kuimba siku hiyo.

Post a Comment

Previous Post Next Post