Himid Mau ala shavu Misri



Uongozi  wa Klabu ya Azam  imebariki safari mpya ya Nahodha wake , Himid Mao Mkami ambaye amesaini mkataba wa miaka mitatu kujiunga na Petrojet ya Ligi Kuu ya Misri.


 Himid ameondoka kwa baraka za uongozi wa klabu ya Azam FC na leo Msemaji wa klabu, Jaffar Idd amesema kuwa msimu ujao hawatakuwa na Nahodha wao huyo.

 “Uongozi sisi hatuna kipingamizi, Himid ni mchezaji wetu wa muda mrefu tokea akiwa mdogo kabisa ameshiriki mafanikio mengi ya timu, mara baada ya kuleta maombi hayo sisi tulimkubalia na tunamtakia kila la kheri huko aendako katika maisha yake mapya,” alisema.

 Wakati huo huo: Azam FC imesema kwamba kocha mpya, Mholanzi Hans van der Pluijm atajiunga na klabu baada ya fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Azam Sports Federation (ASFC) akiiongoza kwa mara ya mwisho klabu yake ya sasam Singida United.

Safari  Himid kwenye ulimwengu wa soka ilianza mwaka 2011 kwenye klabu hiyo upande wa vijana chipukizi.

Post a Comment

Previous Post Next Post