Mama mmoja nchini Marekani amekutana na bintiye, Melissa
Ohden aliyedhani kuwa amefariki dunia miaka 30 iliyopita kutokana na yeye kuitoa
mimba yake.
Mnamo 1977, katika hospitali moja nchini Marekani katika jimbo
la Iowa, Mamake Melissa aliyekuwa na umri wamiaka 19 alitoa mimba kwa kutumia
kemikali kwa zaidi ya siku tano.
Melisaa alizaliwa akiwana miezi minane akiwa na kilo
1.3 na akatupwa kwenye taka taka za hospitali.Hapo ndipo nesi mmoja alisikia
sauti ya mtoto akilia na kwa kuchungulia akaona mwili ukisogea.Melissa
alikimbizwa katika chumba cha wagonjwa mahututi ambapo aliponea na kuishi.
Madaktari walidhani atakuwa hawezi kuona na kwa wakati mmoja
walidhani ataugua matatizo ya moyo yasiotibika.Lakini amefanikiwa kusihi maisha
yenye afya tele na amelelewana familia iliomuasili.
Melissa ambaye ameandika vitabu kuhadithia maisha yake anasema
aligundua kwamba aliasiliwa wakati alipogombana na dadake kutoka familia
iliomuasili.
Chanzo: BBC Swahili
