Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeombwa kuunda tume kwa ajili ya
uchunguzi kwenye kesi ya mauaji ya Bilionea Erasto Msuya.
Ombi hilo limewasilishwa leo Jumatatu Juni 4, na Miriam Mrita Mtuhumiwa wa kesi hiyo
ambaye alikuwa Mke wa Marehemu Msuya Mbele ya Thomas Simba, Hakumu Mkazi Mkuu wa
Mahakama hiyo.
Miriam na Mwengine Revocatus
Muyela wanatuhumiwa kwenye kesi namba 5
ya mwaka 2017 ambapo wanadaiwa kuwa
Tarehe 25 Mwezi Mei 2016 Maeneo ya Kibada , Kigamboni jijini Dar es Salaam walimuwa Aneth Msuya dada wa marehemu Erasto Msuya.
Miriam aliiomba Mahakama
kuundwa kwa tume hiyo kutokana na madai yake kuwa kuna uonevu unaendelea kwenye
kesi hiyo.
Ombi hilo amelitoa baada Patric
Mwita Wakili wa Serikali kuomba kuahalishwa
kesi hiyo kwa madai kuwa jalada halisi la kesi hiyo lipo kwa Mkurugenzi wa Mashtaka
(DPP).
Mwita ameiomba Mahakama
kuihalisha kesi na itajwe tarehe
nyengine ndipo aliponyoosha mkono na hakimu akamruhusu aongee.
"Mimi ni mama mjane, mume
wangu ameuawa, mimi nipo mahabusu gerezani kwa miaka miwili, kama mama sijui
watoto wangu wanaendeĺeaje huko nje,”
“Alichagiza kuchelewaweshwa kwa
upelelezi ambapo kila uchwao anaambiwa upelelezi haujakamilika. "Mtu
ukishafiwa na mume kuna vurugu mechi zinaendelea huko nje, naomba iundwe tume
ya uchunguzi wa kina ya kuichunguza kesi hii kwa sababu kuna uonevu ambao
unaendelea,"Alieleza Miriam.
