Ratiba ya Mazishi ya Sam wa Ukweli hii hapa , Meneja wake asimulia umauti ulivyomfika


Meneja wa  Marehemu Salumu Mohammedi  'Sam wa Ukweli' amri Aliamini amesema marehemu 'Sam wa Ukweli'  atazikwa kesho saa 9 alasiri nyumbani kwao Kiwanga Bagamoyo.

Amri amesema kuwa wanafamilia na wote watakao guswa na kifo cha Msanii huyo aliyetamba na kibao cha sina raha watakutana leo eneo la Tandale Sokoni kwa mjomba  wa Sam wa Ukwel,i Saidi Yanga.

Akisimulia umauti uliomkuta msanii huyo Amri amesema jana tarehe 6 Juni alikuwa studio ya A Sound iliyokuwepo Mabibo kuanzi majira ya saa 2 usiku ambapo kuanzia saa 4 usiku alizidiwa ghafla ambapo waliamkimbiza hospitalini Sinza Palestina .

Amri anaema kuwa kabla hawajafika Hospitali Sam wa Ukweli alikiwa kashapoteza uhai hivyo walifika naye hospitalini Palestina na kujifadhowa kwa muda ambapo baadaye alipelekwa Mwananyamala Hospital .

Amri aliiambia 24SevenUpdater kuwa Sam alikuwa akisumbuliwa na Homa ya manjano na malaria kwa muda wa mwezi mmoja na nusu .

Abdallah Mohamedi Salim ndugu wa marehemu Sam wa Ukweli  amesema kuwa atakayeguswa na msiba huo afike Tandale Hospitali kwa Mjomba wao Saidi Yanga kwaajili ya mipango ya kumujifadhi .

Abdallah amesema kuwa watu watakutana kesho saa mbili asububi kwenye hospital ya Mwananyamara kwa ajili ya kuelekea Bagamoyo Kiwanga kumuhifadhi ndugu yao.


Post a Comment

Previous Post Next Post