Msichana wa miaka 19 aliyehukumiwa kifo akata rufaa

Msichana raia wa Sudan Noura Hussein ambaye alihukumiwa kifo kwa kosa la kumuua mume wake kutokana ya madai kuwa alimbaka amekata rufaa.
"Leo tulikata rufaa kwenye mahakama ya rufaa kupinga uamuzi uliotolewa na mahakama ya chini," wakili wake Al-Fateh Hussein aliliambia shirika la AFP Alhamsi.
Mahakama ya Sudan ilimkuta Bi Hussein na hatia kwa kuua kwa makusudi mapema mwezi Mei baada ya familia ya mumewe kukataa kufidiwa fedha.
Hatma ya Bi Hussein ambaye sasa ana umri wa miaka 19, ilizua maoani kote duniani na hata kuanzisha kampeni #HakikwaNoura
Baba yake Bi Hussein alimalazimisha kuolewa akiwa na miaka 16 na alikua amejaribu kukimbia.
Baada ya ya familia kumkabidhi kwa mume wake, Bi Hussein alisema mume wake aliwaita binamu zake waliomshika huku akimbaka.
Alimdunga kisu na kumua mumewe wakati alijaribu tena kumbaka siku iliyofuati.
Mahaka ya sharia ilimhumu kifo kwa kunyongwa.
Wakati huo huo kundi la wanaharakati wa kupigania haki za kibinaadamu la Equality Now limesema kuwa litamwandikia rais Omar al-Bashir kumuomba amuonee huruma.
Shirika la Amnesty International limesema kuwa hukumu ya mwanamke ya kifo ambaye alikuwa akijitetea inaangazia uzembe wa serikali kukabiliana na ndoa za watoto , ndoa za lazima na ubakaji katika ndoa.

Post a Comment

Previous Post Next Post