Watalii wawili watekwa


Watalii wawili  kutoka Uingereza wameripotiwa kutekwa katika hifadhi ya wanyama ya Virunga nchini DRC.

Taarifa hizo zimetolewa na redio ya Umoja wa Mataifa ambapo kwa mujibu wa taarifa hizo watalii hao wametekwa Kaskazini mwa Kivu wakati wakirudi katika mji wa Goma.

Msemaji wa hifadhi hiyo ya wanyama Joel Wengamulay amesema kuwa aliekuwa akiwasindikiza watali huyo aliuawa wakati watalii hao walpotekwa.

Joel amelaani kitendo hicho na kuahidi kuwa uchunguzi zaidi unaendelea.

Post a Comment

Previous Post Next Post