Spika Ndugai amsurubu Waziri wa Mifugo


Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina  amejikuta akiwa kwenye wakati mgumu kama iliovyokuwa kwa waziri wa Kilomo Charles Tizeba baada ya Spika wa bunge Job Ndugai kutokana wizara hiyo kuruhusu chapa ya moto kwa mifugo.

Hoja hiyo imeibuliwa na Mbunge wa Viti Maalumu Matha Mlata ambaye ametaka Serikali kuachana kabisa na suala la chapa ya mifugo kwa kuwa inaumiza mnyama bila sababu za msingi.

Spika  Ndugai  amesema Wizara imeshindwa kufanya mambo kisomi  hata kufananisha wazee wa zamani ambao waliweka alama mifugo yao na ilitambulika vizuri ingawa hawakuwa wamesoma lakini walithamini mifugo yao na kuwa na huruma.

Katika mchango wake kwa Wizara ya Mifugo, Mlata amesema mambo yanayofanywa na Wizara hayaonyeshi kabisa kama wizara hiyo inaongozwa na wasomi .

“Kuna msomi gani huko wizarani ambaye anaruhusu kuchoma vyuma vya moto na kuwachoma wanyama wetu bila sababu za msingi, hivi hakuna namna nyingine ya kuweka alama hizo?” amehoji Mlata.

Mbunge huyo amepinga suala la operesheni akisema haliko sahihi kwani kuna watu wanaonewa bila sababu za msingi na kwa namna moja linawanufaisha upande wa serikali tu.

Mbunge Innocent Bilakwate amepinga suala la chapa akisema limeumiza mifugo kwa kiasi kikubwa na halina tija yoyote hivyo akawataka wataalamu kubuni mbinu nyingine.

“Haiwezekani hata kidogo kutumia machuma na kuanza kuwaumiza mifugo halafu ninyi mnafurahia, hivi hamulioni hilo kuna wataalamu gani huko jamani,” alihoji.

Mbunge wa Namtumbo Edwin Ngonyani amesema katika eneo lake wameumiza mifugo na chapa hizo hazionyeshi ubora wa aina yoyote zaidi kuacha madonda yasiyotibika kwa mifugo.

Ngonyani amesema Namtumbo wameumizwa pia kwa kusababishiwa migogoro baina ya wakulima na wafugaji baada ya ng’ombe wengi kupelekwa eneo hilo ambalo ni dogo kijiografia.

     

Post a Comment

Previous Post Next Post