Hiki hapa kiapo cha Zitto kwa Familia ya Azory na wengine waliopotea kwenye mazingira tata



KIONGOZI wa chama cha Act-Wazalendo Zitto Kabwe ameendika waraka mrefu mzito wenye ahadi ya kutoacha kupaza sauti yake kutokana na kupotea kwa Mwandishi wa habari nchini Azory Gwanza wa gazeti la Mwananchi

usomee hapa waraka huo wenye ahadi kwa familia ya Azory Gwanda

Leo imetimia miezi 6 tangu yapo mahusiano ya kupotea kwa Azory Gwanda na kazi yake ya Uandishi wa habari, amechukuliwa wakati akifanya uchunguzi mzito juu ya Mauaji  ya Mkiru  (Mkuranga - Kibiti - Rufiji),

Mei 4 nilieleza bungeni juu ya watu 380 wanaodaiwa kuuawa Mkiru , na nilitoa orodha ya awali ya majina 62 ya waliopotea/kuuawa. Na kuliomba bunge lichunguze kupotea kwao, pamoja na Ben Saanane, Simon Kanguye na Azory mwenyewe. Bunge lilikataa kuchunguza.

Leo ikiwa ni nusu mwaka tangu Azory apotee, mkewe, Dada yetu Anna Pinoni aliyekuwa mjamzito, ameshajufungua mtoto wa Kike, tangu Februari, 2018. Binti yao sasa ana miezi mitatu, akilelewa kwa huzuni, upweke, mfadhaiko wa baba yake kutokujulikana aliko.

Ahadi yangu kwa familia ya Azory ni kuwa sitanyamaza, sitaacha kusema, mpaka pale atakapopatikana au Serikali kusema ilipompeleka. Huu ni wajibu wangu kama Mbunge, sitaacha kuutekeleza hata kama Bunge limekataa wajibu wa kuchunguza jambo hili. Pamoja na ahadi hiyo, bado narudia wito wangu nilioutoa jana, siku ilipotimia miezi 10 tangu kupotezwa kwa Simon Kangoye, Diwani na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kibondo kama ifuatavyo:

1. Mosi ni kuikumbusha Serikali juu ya wajibu wake wa kulinda usalama na uhai wa Raia. Serikali ijue hatujasahau, inao wajibu wa kutueleza Azory alipo, maana mara ya mwisho alichukuliwa na Maafisa wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama vya Serikali.

2. Pili ni kulikumbusha Bunge kuwa linao wajibu wa kuchunguza juu ya kupotezwa kwa Azory Gwanda, Simon Kangoye, Ben Saanane, pamoja na watu zaidi ya 380 wa MKIRU. Haswa ikiwa kupotezwa kwao kumehusishwa na Serikali. Bunge haliwezi kukwepa wajibu wake huo.

3. Tatu ni kuwahimiza na kuwakumbusha Watanzania wote umuhimu wa kupaza sauti kutaka Serikali iseme walipo Watanzania wenzetu hawa, na kulitaka Bunge lichunguze juu ya kupotea kwao. Mamlaka na Madaraka ya Uongozi wetu sisi Viongozi yanatoka kwenu wananchi, mnao wajibu wakuonyesha hampendezwi na mambo haya ya watu kupotezwa tu. Mnao wajibu wa kupaza sauti.


Post a Comment

Previous Post Next Post